Hapa tunatoa taarifa kuhusu dalili za magonjwa makuu ya kuambukiza. Ni muhimu kuyatibu magonjwa haya haraka iwezekanavyo. Kuanya hivi kutalinda afya yako na kuzuia watu wengine dhidi ya maambukizo.
Hapa tunatoa taarifa kuhusu dalili za magonjwa makuu ya kuambukiza. Ni muhimu kuyatibu magonjwa haya haraka iwezekanavyo. Kuanya hivi kutalinda afya yako na kuzuia watu wengine dhidi ya maambukizo.
Ikiwa una dalili zozote au unahisi kuugua, wasiliana na wahudumu wa Medic-Help.
Kikohozi kinaweza kuwa ishara ya magonjwa mbalimbali. Mara nyingi kinahusiana na mafua. Wakati mwingine ni dalili ya ugonjwa wa kuambukiza.
Nenda kwenye kituo cha Medic-Help ikiwa unakabiliwa na kikohozi kikali au cha kudumu, au cha kipindi kirefu, au kikohozi kilicho na kohozi.
Kikohozi kinaweza kuwa ishara ya magonjwa mbalimbali. Baadhi ya magonjwa yanayoweza kuashiriwa na kikohozi ni pamoja na:
Ikiwa joto la mwili linazidi kiwango cha kawaida, hii inajulikana kama homa. Kinaweza kuwa ishara ya magonjwa mbalimbali.
Ikiwa una homa, tembelea kituo cha Medic-Help.
Ikiwa mtoto wako ana homa, chukua hatua kwa haraka na umpeleke kwenye kituo cha Medic-Help.
Kunywa maji au chai ya kutosha kwa kiasi kidogo na uepuke kufanya shughuli zinazotumia nguvu nyingi.
Homa inaweza kuwa dalili ya magonjwa mbalimbali. Baadhi ya magonjwa yanayoweza kuashiriwa na homa ni pamoja na:
Ni jambo la kawaida kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku majira ya joto. Hili pia linaweza kufanyika ikiwa chumba cha kulala kina joto jingi. Hata hivyo, ikiwa unatokwa na jasho jingi wakati wa usiku katika halijoto ya kawaida la kawaida, hii inaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa kuambukiza.
Ikiwa una homa kando na kutokwa na jasho usiku, na pia unapoteza uzito, tembelea kituo cha Medic-Help.
Kutokwa na jasho usiku kunaweza kuwa dalili ya magonjwa mbalimbali. Baadhi ya magonjwa yanayoweza kuashiriwa na kutokwa na jasho usiku ni pamoja na:
Ikiwa kuna vipele vya ngozi, mara nyingi madoa au viputo vyekundu hutokea ngozini, au ngozi huwa kavu sana na kubambuka, au huwasha sana. Hii inaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa kuambukiza.
Ikiwa una vipele au kuwashwa ngozi, tembelea kituo cha Medic-Help.
Upele au kuwashwa kunaweza kuwa dalili ya magonjwa mbalimbali. Baadhi ya magonjwa yanayoweza kuashiriwa na upele au kuwashwa ni pamoja na:
Mikato, mikwaruzo au kuumwa kunaweza kujeruhi ngozi na kusababisha vidonda wazi. Vidonda ambavyo haviponi vizuri vinapaswa kutibiwa kwa njia maalum.
Ikiwa una vidonda wazi vya ngozi, tembelea kituo cha Medic-Help.
Mara nyingi vidonda wazi vya ngozi husababishwa na majeraha. Visipopona vizuri, hii inaweza kuwa dalili ya:
Ikiwa unaenda haja kubwa kwa zaidi ya mara tatu kwa siku, au ikiwa unatoa kinyesi kiowevu, una ugonjwa wa kuharisha. Hii inaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa kuambukiza.
Ikiwa unaharisha, tembelea kituo cha Medic-Help.
Kunywa maji au chai ya kutosha kwa kiasi kidogo.
Nawa mikono yako mara nyingi kwa sabuni ili uepuke kuwaambukiza watu wengine.
Kuharisha kunaweza kuwa dalili ya magonjwa mbalimbali. Baadhi ya magonjwa yanayoweza kuashiriwa na kuharisha ni pamoja na:
Kutapika kunaweza kuwa dalili ya magonjwa mbalimbali. Kutapika pia kunaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa kuambukiza.
Ikiwa unatapika, tembelea kituo cha Medic-Help.
Kunywa maji au chai ya kutosha kwa kiasi kidogo.
Nawa mikono yako mara nyingi kwa sabuni ili uepuke kuwaambukiza watu wengine.
Kutapika kunaweza kuwa dalili ya magonjwa mbalimbali. Baadhi ya magonjwa yanayoweza kuashiriwa na kutapika ni pamoja na:
Ikiwa unatatizika kulala kwa siku kadhaa au una hofu isiyoeleweka, hii inaweza kuwa dalili ya dhiki ya akili. Mambo haya hufanyika ikiwa una maumivu yasiyo na kisababishi dhahiri.
Ikiwa unatatizika kulala vizuri au una maumivu yasiyo ya kawaida, wasiliana na Medic-Help.
Matatizo ya kulala, hofu isiyoeleweka au maumivu yasiyo ya kawaida yanaweza kuwa dalili ya magonjwa mbalimbali. Baadhi ya magonjwa yanayoweza kuashiriwa na hali hizi ni pamoja na:
Katika ukurasa huu utapata maelezo zaidi kuhusu magonjwa makuu ya kuambukiza.
Bila shaka, zipo dalili nyingi zaidi. Ikiwa unaugua na una swali linalohusiana na afya, nenda kwenye kituo cha Medic-Help.