Kudumisha afya bora

Ukifuata vidokezo vilivyotajwa hapa chini, unaweza kujikinga dhidi ya magonjwa kadhaa ya kuambukiza.

4A Haende Waschen

Ulinzi rahisi zaidi na fanisi zaidi dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ni kunawa mikono yako kabisa kwa sabuni mara nyingi. Nawa mikono yako angalau kila baada ya kwenda msalani na kabla ya kula.

1D Haende

Oga mwili mara nyingi na upigwe mswaki mara tatu kila siku.

Utunzaji wa mwili wa mara kwa mara hukulinda dhidi ya magonjwa. Wasiliana na Medic-Help ikiwa una maumivu ya meno.

4D Impfung

Watu wanaweza kuyaepuka magonjwa mengi kwa kuchanjwa. Ikiwa watu wengi watachanjwa, basi idadi ya magonjwa itapungua.

Mamlaka ya afya ya Uswisi inapendekeza watu wachanjwe dhidi ya (baadhi ya wengine):

  • Tetekuwanga
  • Surua/matumbwitumbwi/rubela
  • Dondakoo/pepopunda/kifaduro
  • Polio
Icon_Medic_Help.png

Tembelea Medic-Help upate ushauri

4E Geschlechtsverkehr

Pamoja na Ukimwi, kuna magonjwa mengi ambayo yanaweza kuambukizwa kwa ngono. Unaweza kujikinga kabisa kwa kutumia kondomu wakati wa kushiriki ngono. Pia kuna kondomu za wanawake.

Kondomu hupeanwa kituoni au kununuliwa katika duka la dawa au maduka makubwa.

4F Drogenkonsum

Ikiwa unatumia sindano zilizotumiwa kujidunga dawa za kulevya, unaweza kuambukizwa ugonjwa kupitia damu. Kwa hivyo, daima tumia sindano safi na zisizotumiwa.

2C Schwangerschaft

Wasiliana na Medic-Help ikiwa una ujauzito. Mtaalam atajadiliana nawe kuhusu mahitaji yako na unachohitaji kwa ajili yako mwenyewe na mtoto wako ili kudumisha afya bora, na atakupangia miadi ili umwone mtaalamu wa matibabu.

1B Wo Medizinische Hilfe

Hakikisha kuwa watoto wako amechunguzwa mara kwa mara katika kituo cha Medic-Help. Kituo cha Medic-Help pia kinaweza kukusaidia kujibu maswali yanayohusiana na lishe na utunzaji wa mtoto wako. Kwa hivyo, watoto wako wataendelea kuwa na afya bora na kukua vizuri.