Unachoweza kufanya unapougua

Kuna wataalam wa matibabu (Medic-Help) katika kila kituo cha mapokezi na cha matibabu. Shauriana nao ikiwa unatumia dawa, una ujauzito, unahisi kuugua au una maswali yoyote yanayohusiana na afya. Wataalam hawa watakutibu, au, ikiwa itahitajika, watakwandikia rufaa kwa daktari au hospitali.

Ikiwa kituo cha Medic-Help kimefungwa, wasiliana na wasaidizi au wahudumu wa usalama.

Maswali yako yanayohusiana na afya yako na maelezo kuhusu magonjwa yako yatawekwa faragha.

Pia nenda kwenye kituo cha Medic-Help kwanza ikiwa umehusika katika ajali. Nenda hospitalini moja kwa moja ikiwa una tatizo la dharura tu.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa wewe au mtoto wako ni mgonjwa na una swali linalohusiana na afya, nenda kwenye kituo cha Medic-Help.

 

Utunzaji wa kimatibabu katika vituo vinginevyo vya wanaotafuta kimbilio

Wapo wahudumu wa kuwasiliana nao katika kila kituo cha wanaotafuta kimbilio wataojibu maswali yanayohusiana na afya. Utapokea maelezo ya kina kwenye tovuti hii.